Mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums Maxence Melo Aachiwa kwa dhamana
Mwanzilishi
wa mtandao wa JamiiForums Maxence Melo ameachiwa kwa dhamana leo
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukaa mahabusu kwa
takribani siku 5.
Melo
anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kumiliki na kuendesha tovuti
ambayo haijasajiliwa hapa nchini Tanzania (JamiiForums).
Mashtaka
mengine ni kuzuia na kuharibu taarifa ambazo Jeshi la Polisi wamekuwa
wakizitaka kwa ajili ya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria
ya Makosa ya Mitandao na kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la
Polisi na kuharibu uchunguzi chini ya kifungu cha namba 22 cha Sheria
ya Makosa ya Mitandao.
Post a Comment