Mahakama Yaamuru Jide Awaombe Radhi Viongozi wa Clouds
DAR ES SALAAM: Mahakama ya
Wilaya Kinondoni leo Jumatano, Novemba 2, 2016, imemtia hatiani
mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo “Lady Jaydee”
(pichani juu) kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya viongozi wa Clouds
Media Group Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.
Mahakama hiyo imemuamuru aombe radhi
kupitia kwenye chombo cha habari chenye “coverage” kubwa nchini kote na
ikiwezekana duniani.
Joseph Kusaga.
Katika kesi hiyo, Jaydee anashtakiwa na
viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo
Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti wa Redio hiyo, Ruge Mutahaba kwa
kuuchafua uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wake kupitia mitandao ya
kijamii katika malumbano makali kati ya pande hizo mbili.
Ruge Mutahaba.
Mei 2013, Clouds Media Group na Ruge
walimburuza Jaydee mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa
akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.
Katika kesi
inayomkabili msanii Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jay Dee dhidi
ya walalamikaji Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kesi namba 29 ya Mwaka
2013 hukumu yake imetolewa leo na Hakimu wa mahakama ya Wilaya Boniphace
Lihamwike kuwa wameridhishwa na ushahidi uliotolewa kuwa msanii huyo
alitenda kosa la kuwadhalilisha na kuwakebehi kwa maneno machafu ndugu
Joseph Kusaga pamoja na Ndugu Ruge Mutahaba.
Hhivyo Mahakama ya
Wilaya ya Kinondoni imeamuamuru msanii huyo kuomba radhi katika chombo
cha habari cha kitaifa au kinachosikika kimataifa pamoja na duniani
nzima kuwa maneno yake yalikuwa ya kashfa na udhalilishaji yenye lengo
la kuichafua taswira nzuri ya ndugu Kusaga pamoja na ndugu Ruge Mutahaba
vilevile Mahakama imemuamuru Jide msanii huyo kulipa fidia na gharama
za uendeshwaji wa kesi hiyo.
Hukumu ya kesi hiyo
iliyosomwa leo saa 2:30 asubuhi katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni
upande wa Msanii Judith Wambura uliwakilishwa na Wakili wake aitwaye
Advocate Chacha licha ya msanii huyo kuhudhuria mahakamani hapo na
kushindwa kushuka kwenye gari aina ya Noah waliyokuwa wamefika nayo
Mahakamani hapo akiambatana na Meneja wake Seven Mosha ambaye alizuiliwa
getini na walinzi kutokana na kuvaa nguo isiyozingatia maadili ya
Mahakama.
Mwenendo wa kesi
hiyo iliyofunguliwa tangu mwaka 2013 kwa msanii huyo akituhumiwa
kuwatukana, kuwakebehi pamoja na kuwakashifu ndugu Joseph Kusaga pamoja
na Ruge Mutahaba kupitia mitandao ya kijamii na mahojiano aliyokuwa
akifanya mara kwa mara na vyombo tofauti vya habari.
Tangu kesi hiyo
ilipofunguliwa msanii huyo amekuwa na mwenendo usiokuwa wa kuridhisha na
kumfanya kushindwa kesi hiyo ni pamoja na;
1. Kukosa ushahidi wa yale aliyokuwa akiyazungumza yeye binafsi kwamba ametendewa na kufanyiwa na washtaki,
2. Kukosa mashahidi
wa kusimama mahakamani kutetea alichokuwa anakisema kwani mpaka kesi
inamalizika hakuweza kuleta shahidi hata mmoja. upande wa washitaki
uliweza kuleta mashahidi takribani 15 mpaka hukumu ya kesi inasomwa hii
Leo.
3. Kutokuhudhuria
mahakamani yeye mwenyewe, jambo linalotafsiriwa na wengi kama kutokuwa
makini lakini pia kukurupuka kwa yale aliyokuwa akiyasema na kuandika
kwani inawezekana kabisa sababu tajwa hapo juu zilimfanya aingie mitini.
Moja kati ya maneno yaliyomtia hatiani Jaydee ni wosia aliouandika May 2013 kupitia blog yake.Wosia huo ulisomeka:
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye
maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi. Na bado
naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa
mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa
vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye
ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo
cha habari. Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao
kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya
muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa
baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua
kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote
unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna
msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao
mnaofikiria. Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo
influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta
nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na
kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na
kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU
alizonipangia. Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao
hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku
nitakapokuwa nimekufa. Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao. Natambua
wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu
alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka
jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa
CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na
kifo changu. Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na
mkiwaona muwapige. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu. Kama wamenifitini,
na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa
marehemu. Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya
wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta
pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi
na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini
sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album
yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya
Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku
yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka. Na hii ni kwasababu
wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki
dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama
mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio
nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu. Mnawatishia wasanii kuwa
yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa
kunijadili. Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine
wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani,
Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi?? Ilikuwa
niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari
yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili. Kila siku
mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge,
watu hamjui tu. Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide
inakuuma?? Roho gani hiyo?? Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu.
Licha ya hukumu hiyo kutolewa, Meneja
wake, Seven Mosha, amesema kuwa Lady Jaydee atatoa maelezo yake kuhusu
hukumu hiyo muda si mrefu.
Post a Comment