Picha: Mamia wajitokeza kumzika Thomas Mashali
Mamia ya watu Jumatano hii wamejitokeza kumzika bondia, Thomas Mashali aliyeuwawa usiku wa kuamkia Jumatatu kwa kupigwa na watu baada ya kudaiwa kuitiwa kelele za mwizi, kwa mujibu wa taarifa ya mtu wake wa karibu
Mashali ambaye alitambulika zaidi kimapigano kama ‘Simba wa Nyika’ amezikwa katika makaburi ya Kinondani jijini Dar es salaam.
Kwa sasa familia inasubiria ripoti ya polisi huu kifo cha Mashali.
Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) Yassin Abdallah (Ustadh) akizungumza na waandishi wa habari juu ya kifo cha Thomas Mashali
Bondia Japhet Kaseba (katikati) akizungumza na wadau wa ndondi
Mashabiki wa ngumi wakipiga picha mbele ya kaburi la Mashali
Wadau mbalimbali wa ndondi wakijadiliana mambo baada ya mazishi
Post a Comment