KESI YA SIMBA NA YANGA KUHUSU KESSY YAAHIRISHWA
Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iimeahirisha kikao chake
kilichokuwa kikae kesho Jumapili Septemba 4, 2016 kutoa hukumu ya shauri
la mchezaji Hassan Ramadhan Kessy anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja
mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na klabu ya Young Africans sambamba
na kusajili katika timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya
mkataba wake kufika mwisho Juni 15, 2016.
Simba imelalamika mbele ya kamati hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa, mchezaji Hassan Kessy alivunja taratibu hizo akiwa ndani ya mkataba wa klabu hiyo yenye mashakani yake Barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati hiyo, shauri hilo lilisikilizwa baadaye mwezi huu katika tarehe itakayopangwa hapo baadaye. Sababu za kuahirisha kikao hicho ni kutotimia kwa akidi ya wajumbe wa kamati nzima. Akidi ni lazima wajumbe zaidi ya watatu wathibitishe kushiriki.
Ilikuwa isikiliwe kesho baada ya kushindikana kusikilizwa kwa shauri jingine linalohusu Klabu Simba ikiilalamikia Klabu Young Africans, kuingia mkataba na mchezaji Hassan Ramadhani Kessy wakati bado ana mkataba na klabu Simba.
Shauri la Simba dhidi ya Young Africans lilishindika kusikilizwa kwa sababu Young Africans hawakutokea mbele ya kamati hiyo wakati wa kusikiliza shauri hilo, hivyo kamati itaiandikia barua Young Africans kukumbushwa kuhudhuria kwenye kesi hiyo Jumapili ijayo kabla ya kutolewa uamuzi.
Kama
hawakutokea tena, shauri hilo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa
uamuzi upande mmoja. Kadhalika mashauri mengine yatakayosikilizwa hapo
baadaye ni pamoja na yale ambayo wahusika walipewa nafasi ya kuyamaliza
nje ya kamati lakini wakashindwa.
Post a Comment