Picha: Wasanii wa WCB walivyopokelewa Lodwar, Kenya
Siku mbili zilizopita wasanii wa lebo ya WCB, Harmonize, Raymond na Rich
Mavoko waliwasili nchini Kenya kwa ajili ya kufanya show nchini humo
pamoja na kufanya ziara kwenye vituo mbalimbali vya habari vilivyopo
huko.Wasanii hao walipata mapokezi ya heshima mjini Lodwar, Kenya japo siyo
rahisi kwa wasanii kama wao ambao hawana muda mrefu kwenye muziki
kutegemea kufanyiwa hivyo japo Rich Mavoka inadaiwa kuwa ni mmoja kati
ya wasanii wa Bongo wanaokubalika nchini humo.
Wananchi wa mji huo wanaonekana kuwakubali zaidi wasanii wa Bongo ikiwa
ni wiki mbili zilizopita Mr Nice alifanikiwa kupata mapokezi ya kishindo
kwenye mji huo huo. Wasanii hao walifankiwa kufanya show usiku wa jana,
Septemba 2 kwenye ukumbi wa Home Land Club.
Post a Comment