Wanataka kuniua - Saida Karoli
Ikiwa imepita miezi miwili toka msanii wa nyimbo za asili Tanzania Saida Karoli arudi rasmi kwenye muziki na kuachia kazi zake mbili zilizopata mafanikio na kuwafikia watu wengi zaidi ameibuka na kudai watu wameanza kumpiga vita kishirikina na wanataka kumuua
Saida Karoli ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Orugambo' amedai kuwa ushirikina upo na watu wanampiga vita ili aweze kupotea tena kwenye muziki kama ilivyotokea kipindi cha nyuma na kudai kuna mtu amelipwa pesa ili amuuwe kabisa jambo lililopelekea kuahirisha baadhi ya show zake.
"Huyo mtu alinielekeza watu kadhaa ambao wamepanga mpango wa kuniua aliniambia, sasa mimi nimeshalipwa nikuuwe nikuondoe duniani kabisa yaani kabla ya kufika Mwanza, Geita tena bora hata hizi show zingine uvunje, kweli ramani aliyonipa nilichoka ikabidi show zingine za Bukoba tumezivunja tukasema ngoja tutulie kwanza tuone nini kitaendelea" alisema Saida Karoli
Saida Karoli anakiri wazi kuwa suala la ushirikiana lipo na kwake si jambo la ajabu kumtokea kwani tayari ameshakutana na mambo ya namna hiyo sana na kudai yeye anamtegemea Mungu na kumuomba Mungu.
Post a Comment