Museveni Rasmi Apinga Ushoga
PAMOJA na kulaumiwa kwa mambo mabaya mengi, hasa ya kuminya
demokrasia nchini Uganda, Rais Yoweri Kaguta Museveni ameweza kufanya
kilichowashinda marais wengi wa Afrika.
Rais Museveni amewezesha na hatimaye kupitisha sheria rasmi ya mambo yote yanayohusiana na ushoga nchini Uganda.
Vita ilikuwa kali kutoka mataifa ya magharibi na yenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani ambayo yanaunga mkono suala la ushoga, pamoja na vitisho vingi lakini bado alishikilia msimamo wake.
Wengi wa viongozi wetu wa Kiafrika hawako tayari kuona ushoga unashamiri kwenye nchi zao, hawapendi kabisa lakini misaada inawaponza, wakitishwa kidogo tu wanakaa kimya huku wakikwepa kabisa kulizungumzia suala hilo.
Misaada! misaada! misaada! Ndiyo pingu na gereza la kuifunga Afrika mpaka inashindwa kujiamulia mambo yake mengi kwa uhuru na uwazi.
Pongezi kwako Yoweri Kaguta Museveni. Tunasubiri kuona wengine wanafuata nyayo zako.
Na Leonard Msigwa/GPL

Post a Comment