WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY AKUTANA KWA MARA YA KWANZA NA VIONGOZI WA DUNIA
Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi.
Theresa May, amekutana kwa mara ya kwanza na viongozi wa mataifa
mbalimbali katika mkutano wa G20, tangu achaguliwe kutwaa wadhifa huo
baada ya Uingereza kupiga kura ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.
Waziri Mkuu Teresa May akisalimiana na rais Xi Jinping wa China
Waziri Mkuu Teresa May pia alikutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Saudi Arabia.
Hata hivyo mkutano huo uliibua hisia
za machungu kwa Uingereza pale rais, Barack Obama, aliposema
Uingereza haitapewa kipaumbele cha kwanza katika makubaliano ya
kibiashara na Marekani, kufuatia kujitoa Umoja wa Ulaya.
Waziri Mkuu Teresa May akisalimiana na rais Vladimir Putin wa Urusi.Waziri Mkuu Teresa May akisalimiana na rais Xi Jinping wa China
Post a Comment