Mabasi Yaliyofungiwa Yaanza Kuachiwa
MABASI
yanayosafirisha abiria wanaokwenda mikoani yaliyofungiwa na Serikali
kwa kusababisha ajali yameanza kuruhusiwa kutoa huduma hiyo.
Mabasi
hayo yameruhusiwa baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu
na Majini (SUMATRA) na Wamiliki wa Mabasi ya Abiria (TABOA) kufikia
muafaka.
Makubaliano
hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yalilenga kuleta suluhu
kwa kuwataka TABOA kusimamisha mgomo wa mabasi uliopangwa kufanyika nchi
nzima Agosti 22 mwaka huu.
Zaidi
ya mabasi 60 ya kampuni tofauti yalifungiwa na Serikali baada ya kile
kilichodaiwa na serikali kwamba yalisababisha ajali kwa uzembe wao.
Wamiliki
wa mabasi hayo walikuwa wanahoji sababu ya SUMATRA kufungiwa leseni ya
usafirishaji kwa kampuni badala ya kupewa adhabu basi moja lililopata
ajali badala ya kufungiwa kampuni nzima.
Katibu
Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu jana alisema wamekubaliana mabasi ambayo ni
mazima yaliyofungiwa yaachiwe kutegemeana na utaratibu wa ukaguzi yaweze
kuingia barabarani kutoa huduma ya usafirishaji.
“Tulikubaliana
na serikali ndani ya siku saba iwe imeyafungulia mabasi yetu mazima
kutegemeana na utaratibu wa ukaguzi yaendelee kutoa huduma kwa wananchi
na tayari serikali imeanza kuyaachia baadhi ya mabasi hayo,
“Baadhi
ya mabasi yaliyofungiwa ambayo yameachiwa kutoa huduma ni ya Mohammed
Trans, Mbazi, Kisbo Safari, City Boy, KVC, Wibonera na Kandahari”, alisema Mrutu.
Alisema
walikubaliana serikali iyakamate mabasi yote madogo nchini yanayofanya
safari za usafirishaji abiria mikoani bila ya kuwa na leseni ya biashara
hiyo.
Alisema
mabasi hayo yamekuwa kero kubwa kwa kugombania abiria na yanapokuwa
barabarani yanawachomekea madereva wa mabasi makubwa.
Pia aliomba idadi ya vituo vya polisi vya ukaguzi barabarani vipungue.
Post a Comment