Makundi ya Europa League Haya Hapa, Samatta Awakwepa Man U
Makundi ya Klabu ambazo
zitacheza Europa League ikiwemo timu anayoichezea Mtanzania Mbwana
Samatta, KRC Genk ya Ubelgiji yamepangwa huku matarajio ya Watanzania
wengi ilikuwa ni kumuona pengine Genk ya Samatta wakipangwa kundi moja
na Manchester United wanayoichezea Zlatan Ibrahmovic na Paul Pogba.
Genk na Man U wamekwepana kwa Man U
kupangwa Kundi A huku Genk wakiwa wamepangwa Kundi F. Endapo akina
Samatta watafuzu kwenye kundi lao pia Man U nayo ikafuzu huenda
wakakutana hatua yeyote ya mbele ya mashindano hayo, hivyo Watanzania
watamuona Samatta akimenyana na akina Pogba na Zlatan.
Post a Comment