Pichaz: Ukweli Kuhusu Mapambano ya Polisi na Majambazi Vikindu
Baada ya jambazi huyo kumuua askari, jeshi la polisi liliongeza nguvu eneo hilo na kupiga mabomu na risasi nyingi hewani zilisababisha taharuki katika eneo hilo na kusababisha kila mmoja aseme lake.
Mapaparazi wetu baada ya kufika eneo hilo walitaka kuzungumzia na maofisa wa polisi waliokuwa eneo hilo akiwemo, RPC wa Pwani, Bonaventura Mushongi, Gilles na Kamishna Mwandamizi wa Jeshi hilo, Liberatus Sabas lakini wote walisema hawawezi kuongea chochote mpaka wapate ruhusa kutoka ngazi za juu kwa kuwa tukio hilo si la Kimkoa bali ni la Kitaifa.
Licha ya viongozi hao kukataa kuzungumza, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili ambaye alikuwa bega kwa bega na askari hao alisema kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wanaume 7 ambapo walikutwa wanaume 3 na wanawake 3 ambapo mwanaume mmoja aliyetajwa kumuua Afisa huyo wa Polisi alitoroka pamoja na silaha yake.
Hakuna Jambazi yeyote aliyeuawa katika tukio hilo zaidi ya afisa huyo wa polisi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili
Angalia picha
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/ ISSA MNALLY /GPL.
Post a Comment