Polisi Yakabiliana na Majambazi, Mkuranga
Mapigano makali yanaendelea kati
ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu,
wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.
Magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.
Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru zimefungwa kutokana na mapambano hayo.
Aidha
taarifa za awali ziliripoti kuwepo na majibizano ya risasi kati ya
jeshi la Polisi na watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi maeneo ya
Vikindu, mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo na inadaiwa kuwa askari mmoja
ameuawa kwenye mapigano hayo.
Chanzo: Mwananchi.
Post a Comment