Chama Shujaa Simba Afunga Mabao Mawili Dhidi Ya Power Dynamos
KIUNGO mwenye ufundi mwingi mguuni, Clatous Chama, jana aliibuka shujaa ndani ya kikosi cha Simba baada ya kufunga mabao mawili katika sare ya 2-2 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.
Chama alifunga
mabao hayo dakika ya 58 na 90+2, yote yakiwa ni ya kusawazisha baada ya Power
Dynamos kutangulia wakati wote.
Mchezo
huo uliochezwa Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola, Zambia, Simba ilikuwa na wakati
mgumu baada ya wenyeji wao kupata bao dakika ya 28 na hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika, matokeo yalikuwa Power Dynamos 1-0 Simba.
Wakati watu
wakidhani mechi imelala kwa Simba kupoteza, lakini haikuwa hivyo kwani Chama
tena aliwainua mashabiki vitini katika muda wa nyongeza baada ya tisini
kukamilika.
Bao
hilo liliibua matumaini ya Simba kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa
Afrika msimu huu ambapo malengo yao makubwa ni kucheza nusu fainali ya michuano
hiyo ambapo msimu uliopita waliishia robo fainali.
Simba
wana wakati wa kujiuliza katika mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos
utakaochezwa Oktoba Mosi, mwaka huu jijini Dar ambapo wanahitaji ushindi wa
aina yoyote, sare ya bao 1-1 au 0-0 ili kutinga hatua ya makundi.
chanzo: globalpublishers
Post a Comment