WAKATI TSHISHIMBI AKIWA GUMZO BONGO, SAMATTA AWAKUMBUKA KINA BOBAN, CHUJI
Mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta, Ijumaa hii alitumia ukurasa wake wa Twitter kuwakumbuka wachezaji waliowahi kufanya vizuri kwenye soka la Tanzania miaka kadhaa iliyopita.
Samatta ameandika ujumbe mfupi kwa kusema: “Chuji, Nurdin Bakar, Henry Joseph, Boban, Godfrey Bonny, Humud, Nizar, Babi..na wengine wengi sana leo sijui wangenunuliwa bei gani.”
Ujumbe huo wa Samatta kuhusu viungo hao wa zamani na ambao baadhi yao bado wanacheza soka haijajulikana anawalenga kina nani kutokana na soko la sasa lilivyo.
Kwa sasa kiungo gumzo chini Tanzania ni Papy Tshishimbi wa Yanga ambaye ametua hivi karibuni na kujiunga katika timu hiyo, Tshishimbi alionyesha kiwango kizuri katika mchezo dhidi ya Simba, Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa.
Post a Comment