SINGIDA UNITED YAZIDI KUJIIMARISHA, YAINGIA MKATABA WA MILIONI 250 NA KAMPUNI YA YARA
Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakitia saini karatasi ya makubaliano ya udhamini wa timu ya Singida wenye thamani ya Milioni 250.
Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakibadilishana nyaraka za mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.
Wachezaji wa Singida United wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexande Macedo (kulia) kocha mkuu wa timu ya Singida United Hans Van De Pluijm (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United Festo Sanga.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Timu ya Singida United imeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250 na kampuni ya uzalishaji mbolea ya YARA ikiwa ni katika mikakati ya kuongeza vyanzo vya mapato ya timu hiyo.
Mkataba huo umesainiwa leo mbele ya waandishi wa habari ukishuhudiwa na kocha mkuu wa timu ya Singida United Hans Van De Pluijm.
Akizungumza kabka ya utiaji saini wa Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga amesema kuwa mkataba huu wa mwaka mmoja utaizidi kmuimarisha timu yao katika masuala ya kifedha na zaidi wataendelea kuwakaribisha makampuni mengine kwa ajili ya kufanya nao kazi.
Sanga amesema kuwa, katika moja ya makubaliano yaop wameshapata shamba la ekari 10000 kwa ajili ya kilimo cha Mahindi na zitasimamiwa na kamouni ya YARA ikiwemo uwekezaji wa mazao hayo ndani na nje ya nchi.
Pia mbali na hilo, Singida United wameingua makubaliano ya kibiashara ya kusambaza bidhaa za YARA ndani ya nchi ikiwemo na kuzitangaza.
Kwa upande wa kampuni ya YARA, Mkurugenzi Mkuu Alexander Macedo amesema kuwa wameamua kuidhamini timu ya Singida United kwani wameona ni timu nzuri na hata nembo ya timu yao ina ua la Alizeti ambalo linatumika sana kwa ajili ya utengenezaji mafuta hayo.
Macedo mwenyeji wa Brazili amesema watashirikiana na timu yya Singida ili waweze kuendeleza kilimo cha Mahindi nchini pampja na kuhakikisha wanawapatia wataalamu wazui wa soka kwa ajili ya mafunzo mbalimbali.

Post a Comment