IDARA YA UHAMIAJI:MGOMBEA URAIS WA TFF WALLACE KARIA NI RAIA HALALI WA TANZANIA
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanga
Idara ya Uhamiaji Nchini imethibitisha kuwa Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace John Karia ambaye ni Mgombea Urais wa TFF katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika August 12 mwaka huu ni Raia halali wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi habari makao makuu ya Idara hiyo, Msemaji Mkuu wa Uhamiaji, Ally Mtanga amesema kuwa mmoja wa wagombea wa Urais wa TFF alimkatia rufaa mgombea mwenzake Wallace Karia kuwa si raia wa Tanzania hali ambayo inafanya akose sifa ya kuwa mgombea wa kiti hicho.
"Wallace Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357(Rejeo la 2002) na kanuni zake, wakati huo huo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi".
Mtanga amesisitiza utambuzi wa uraia upo kisheria sura ya 357 (rejeo la 2002} uraia hauangaliwi Rangi, kabila wala dini.
Idara hiyo imevitaka vilabu vyote na taasisi za michezo kuhakikisha wafanyakazi wote na wachezaji ambao raia wa kigeni wanatimiza taratibu zote za kisheria za kukaa nchini bila kufanya hivyo sheria itashika mkondo wake .
Post a Comment