MAOMBI YA DHAMANA YA MANJI KUSIKILIZWA AGOSTI 7 MWAKA HUU.

Mfanyabiashara Yusuf Manji akirudishwa mahabusu baada ya kesi yake ya maombi ya dhamana kuahirishwa hadi Agosti 7mwaka huu.



Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Leo imeahirisha kesi maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na   Mfanyabiashara maarufu Tanzania Yusuf Manji, hadi Agosti 7 mwaka huu kwa kuwa Jaji Isaya Arufani anayesikiliza kesi hiyo anaudhuru.

Kesi hiyo imeahirishwa na  Msajili wa Mahakama kuu siani

Hata hivyo kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, upande wa Mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Paul Kadushi akisaidiana na Simon wankyo wamewasilisha kiapo kinzani kupinga maombi hayo ya dhamana wakiwa na hoja tatu.

Hoja hizo ni kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo ya dhamana, na kwamba upande wa utetezi umewasilisha maombi hayo ya dhamana kwa kutumia vifungu ambayo siyo sahihi kisheria na pia viapo walivyo viwasilisha vina dosari kisheria.

Hata hivyo, kwa kuwa Jaji husika anayesikiliza kesi hiyo hayupo, kesi hiyo itakuwa tena Agosti 7 (Jumatatu).
Katika maombi hayo ya dhamana, Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurgenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Kwa mujibu wa hati ya maombi hayo, Manji anadai kuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo  na kwamba ameambatanisha vyeti vya daktari katika maombi yake.

Katika kesi ya msingi,  Manji na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na mihuri ya mbalimbali ya JWTZ isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.

Mbali na Manji, washtakiwa wengine ni,  Ofisa Rasilimaliwatu Deogratias Kisinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Mtunza Stoo msaidizi, Thobias Fwele (43).

No comments

Powered by Blogger.