Mahakama Kuu Dar leo imetupilia mbali maombi ya wabunge Viti Maalum 8 wa CUF waliofukuzwa.

             Waliokuwa wabunge wa viti maalum wa Chama cha Wananchi (CUF).

Mahakama Kuu ya Tanzania leo tarehe 4 Agosti 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge nane wa viti Maalum kupitia chama cha Chama Cha Wananchi (CUF) ambao wamefukuzwa uanachama na kuipinga kuapishwa kwa wabunge wengine wateule wa chama hicho.
 Wabunge hao nane wa CUF ambao wapo upande wa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad waliamua kwenda mahakamani kupinga kuapishwa kwa wabunge wengine nane wa viti Maalum kupitia chama hicho ambao wametangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) Julai 27, 2017 kwa kile wanachodai kuwa mamlaka zilizowavua ubunge wao si mamlaka halali za CUF. 
Wabunge hao waliofungua kesi kupinga kuapishwa kwa wabunge wateule wa CUF ni pamoja na 
- Mhe. Severina Mwijage    (Mbunge)
- Mhe.Saumu Sakala         (Mbunge)
- Mhe.Salma Mwassa        (Mbunge)
- Mhe.Riziki Ngwali            (Mbunge)
- Mhe.Raisa Mussa           (Mbunge)
- Mhe.Miza Haji                 (Mbunge)
- Mhe.Hadija Ally Al-Qassmy (Mbunge)
- Mhe.Halima Mohamed        (Mbunge)
Katika kesi ambayo ilikuwa imefunguliwa na Wabunge hao nane wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Wananchi CUF ilikuwa ikiongozwa na mawakili wa CUF ambao walikuwa wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala. 

No comments

Powered by Blogger.