KAMBI YA MORO IMENOGA, YANGA YASHINDA 5-0, NGOMA, TAMBWE WATUPIA
Mwanamuziki Pepe Kale ambaye kwa sasa ni marehemu aliwahi kuimba, Yanga Afrika Yanga Moja ya Maitaifa, hilo jina la YANGA WA KIMATAIFA linaweza kuendelea kutokana na aina ya mazoezi ambayo timu hiyo inafanya.
Kwa sasa Yanga ipo kambini Bingwa mkoani Morogoro, ambapo mazoezi ni makali na wachezaji wanaonekana kufurahia mazoezi yanavyoendelea na tayari wameonekana kuwa fiti.
Chini ya Kocha George Lwandamina, Yanga imefanikiwa kuifunga timu ya Moro Kids mabao 5-0 katika mchezo wa kirafiki uliocheza kwenye Uwanja wa Highland Parl unaomilikiwa na Chuo cha Biblia Baptist ambapo ndipo Yanga wanapofanyia mazoezi.
Katika mchezo huo uliotumika kama sehemu ya mazoezi, mabao ya Yanga yamefungwa na Donald Ngoma aliyefunga mawili, Raphael Daudi, Amiss Tambwe na Yusuph Mhiru.
Post a Comment