IGP SIRRO AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KITUO CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI NA NCHI JIRANI CHA UBUNGO


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro (katika) alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo na kituo cha daladala cha Mbezi Luisi, (kushoto) ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP) Murilo Jumanne Murilo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ( katika) akiwa katika ukaguzi wa kushtukiza kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es salaam, Naibu Kamishna wa Polisi ( DCP) Lucas Mkondya akifuatiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Awadhi Haji.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimuelekeza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Muslim kuhakikisha kuwa magari na mabasi yote ya abiria yanakaguliwa mara kwa mara. IGP Sirro alifanya ukaguzi wa kushtukiza jana katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo na Kituo cha Daladala cha Mbezi Luis.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na madereva wa mabasi ya abiria pamoja na abiria wanaosubiri usafiri wa kwenda mikoa mbalimbali na nchi jirani baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, pamoja na kituo cha daladala cha Mbezi Luis.



Na Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka madereva na wamiliki
wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na wamiliki na
madereva wa mabasi madogo ya abiria maarufu kama daladala kuhakikisha
wanayafanyia ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara magari yao ili
kupunguza ajali zinazosababishwa na ubovu na uchakavu wa magari.

IGP Sirro aliyasema hayo jana wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika
Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na kituo cha
daladala cha Mbezi Luisi kwa lengo la kuangalia hali ya usalama wa kituo hicho,
kuona namna ukaguzi wa mabasi ya abiria unavyofanyika kabla hayajaanza
pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za abiria.

“Nimefarijika kuona watendaji wa kituo hiki pamoja na askari wangu wakifanya
kazi vizuri kwa ushirikiano mkubwa hali inayosaidia kupunguza kero mbalimbali
kwa watumiaji wa kituo hiki” alisema IGP Sirro.

Aliongeza kuwa Ubungo ni salama na itaendelea kuwa salama kwa sababu
vibaka wamepungua na wale wanaofanya utapeli katika kituo hicho waache mara
moja na kutafuta kazi nyingine kwa kuwa mwisho wa siku wataacha familia zao
baada ya kukumbana na mkono wa sheria.

Pia ameelekeza magari yote ya abiria yabandikwe namba simu zote za
makamanda wa mikoa wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Wakuu wa
Polisi wa wilaya zote sehemu ambazo itakuwa ni rahisi kuonekana na abiria ili iwe
rahisi kwao kutoa taarifa pindi wanapoona dereva anaendesha gari kwa kukiuka
sheria na kanuni za usalama barabarani.

Aliwataka wananchi kuendelae kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa
za uhalifu na wahalifu ikiwa ni pamoja kutii sheria bila shuruti na kutoa wito kwa
wamiliki wa magari, madereva pamoja na abiria kuwa wastaabu na kuhakikisha

wanaheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani kwa kuwa kila mmoja
anafahamu madhara ya ajali.

No comments

Powered by Blogger.