WAZIRI LUKUVI AWAREJESHEA VIWANJA WATU 180 WALIODHULUMIWA ARDHI

                                                              Waziri William Lukuvi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amefuta hati za viwanja 180 na kuvirejesha viwanja hivyo kwa wamiliki wake halali, waliokuwa wamedhulumiwa haki zao na viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini, kwa kushirikiana na watu wenye fedha.

Waziri Lukuvi ameyazungumza hayo, leo, Agosti 2, ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea matokeo ya oparesheni maalum za kushughulikia matatizo ya ardhi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Waziri Lukuvi amesema katika awamu ya kwanza, waliwasikiliza watu 200 wenye matatizo ya kudhulumiwa ardhi kwenye maeneo ya Kinondoni, Kibaha, Mkuranga na Bagamoyo, awamu ya pili ikahusisha wakazi 100 wa Temeke na Kigamboni huku awamu ya mwisho, ikiwahusisha watu 100 kutoka wilaya ya Ilala.

Waziri Lukuvi amesema katika kuwasikiliza watu hao, wamebaini kwamba kwa kipindi kirefu kulikuwa na mchezo wa wamiliki halali wa ardhi kutapeliwa viwanja vyao na viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini, kwa kushirikiana na watu wenye fedha.

No comments

Powered by Blogger.