HAJI MANARA AZUA GUMZO, AIWAKILISHA YANGA KWENYE UZINDUZI

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara aliibuka na kwenda kuwa mwakilishi wa watani wao wa jadi Yanga wakati Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara walipokuwa wakigawa vifaa kwa timu 16 zitakazo shiriki VPL 2017/2018.
Manara ambaye alikuwa anaiwakilisha Simba katika zoezi hilo, alisimama kwenda kuiwakilisha klabu ya Yanga baada ya mabingwa hao kukosa mwakilishi.
Wanamitindo waliovalia jezi za Yanga  zitakazotumiwa msimu ujao walipanda kwenye jukwaa lakini alipoitwa mwakilishi kutoka Yanga hakuwepo ndipo Manara akaenda jukwani kuwawakilisha watoto wa Jangwani.
Ikumbukwe klabu za Simba na Yanga ni mahasimu uwanjani lakini nje ya uwanja mashabiki wa klabu hivi ni watani na wamekuwa wakitaniana kwa mambo mengi kitu kinacho tia chachu pindi timu hizi zinapokutana uwanjani.

No comments

Powered by Blogger.