CUF WAZICHAPA KAVUKAVU MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DSM

                                              Vurugu zikiendelea mahakamani hapo.

Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba na wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif, wamezichapa konde Mahakama Kuu Kanda ya Dar leo wakati wa kesi ya wabunge waliofutwa uanachama
                                      Wabunge wa CUF waliovuliwa uanachama.

Katika kesi hiyo, wabunge wanane wa CUF waliovuliwa uanachama Prof. Lipumba, inayosikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo, wabunge hao waliiomba mahakama hiyo kuweka zuio la wabunge wapya kuapishwa hadi kesi ya msingi waliyofungua itakapoamuliwa.
                                                Taharuki ikitanda ndani ya mahakama.

Aidha wabunge hao waliiomba mahakama kuzuia utekelezaji wa Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kuwavua uanachama.Kesi hiyo inatarajiwa kutolewa uamuzi leo amahakamani hapo.
                                                        Vurugu zikiendelea za wafuasi wa CUF.

No comments

Powered by Blogger.