AZAM WAMPA PLUIJM BONGE LA KIUNGO

                                                 Mholanzi, Hans van Pluijm.
KLABU ya Azam, imekubali kumuachia kiungo wake mkabaji, Mudathir Yahya kujiunga na kikosi cha Singida United kinachonolewa na Mholanzi, Hans van Pluijm kwa ajili ya kukitumikia kwenye msimu ujao.

Ujio wa kiungo huyo ndani ya Singida United unaweza kumkosha Pluijm ambaye mara kadhaa wakati akiwa kocha wa Yanga aliwahi kuifukuzia saini yake, lakini ikawa ngumu kuinasa.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema, mbali na kumpeleka kiungo huyo kwenye kikosi cha Singida United, lakini kuna nyota wao wengine wamewapeleka timu zingine za ligi kuu kwa lengo la kuwaweka fiti zaidi.

Idd aliwataja wachezaji wengine waliowatoa kwa mkopo ni mlinda mlango, Metacha Mnata aliyepelekwa Mbao FC, mabeki Godfrey Elias na Abass Kapombe (Ndanda FC) na Joshua Thawe aliyekwenda Njombe Mji.
Katika hatua nyingine, Mudathir amesema: “Natafuta sehemu ya kucheza, naamini nikiwa Singida nitapata nafasi hiyo baada ya kuikosa Azam.”

No comments

Powered by Blogger.