AJALI ZA BARABARANI ZINAWEZA KUPUNGUA KWA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI-KAMANDA MUSLIM

 Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akizungumza na waandishi habari katika uzinduzi wa uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
 Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkazo na maagizo ya Ukaguzi wa magari katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix (katikati) akizungumza na waandishi  habari kuhusu ukaguzi magari yanayotoka kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akiweka namba maalmu za simu katika basi itakayotumika kupiga kwa  abiria kwa dereva atakaye kiuka sheria za usalama barabani .
Askari wa Usalama barabani  wakiwa katika ukaguzi mbalimbali wa mabasi katika kituo Kikuu cha Mabasi  Ubungo.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa ajali za barabarani zinaweza kupungua kwa madereva  kufuata sheria za usalama barabarani.
Hayo ameyasema Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim wakati akizindua uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani leo katika kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa namba za simu katika mabasi hayo zitatumika kwa abiria kutoa taarifa ya dereva anaendesha bila kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo mwendo kasi.Kamanda Muslim  amesema kuwa namba hizo ni bure na kwa abiria, dereva au kondakta atakaeng’oa namba hizo atachukuliwa hatua ikiwemo kunyanganywa leseni.
Amesema uwekaji wa namba maalumu kwenye mabasi unafanyika nchi nzima ikiwa yote nikulinda maisha ya abiria katika kuwa na uhakika wa safari zao.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo amesema kuwa watasimamia maagizo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro ambapo yamekaziwa na Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim.
Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix amesema kuwa kila siku wanafanya ukaguzi na gari ambayo ina kasoro haiwezi kufanya safari zake.Amesema watahakikisha kuwa kila basi linalondoka katika kituo cha ubungo linakuwa na namba maalum za simu  katika kila basi.

No comments

Powered by Blogger.