Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu lazinduliwa Zanzibar

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ndege wakati akizindua Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu (STEM) kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed  Shein hapo Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni.
 Balozi Seif akizindua Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu (STEM) kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed  Shein.
 Baadhi ya wageni na walikwa kutoka Chuo Kikuu cha cha George Mason cha Nchini Marekani wakishuhudia  uzinduzi wa Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu.
 Balozi Seif akisalimiana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Profesa Mshimba nje ya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi wakati wa mwanzo wa mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wa Hesabu Tanzania, Mwalimu Said Sima.
Mkuu wa Timu ya Wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha George Mason Nchini Marekani Profesa Padu kati kati akimpatia maelezo Balozi Seif  juu ya ufundishaji wa masomo ya Sayansi, Teknolojia na Hesabu kwa wanafunzi wa Fani hiyo. Nyuma ya Profesa Padu ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uwezeshaji kwa wote Zanzibar iliyoandaa Mafunzo hayo ya STEM  Bibi Giftness Castico. Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments

Powered by Blogger.