Rasmi: Ommy Dimpoz asaini RockStar4000, afunguka haya

                                                  Ommy Dimpoz akisani RockStar4000
 Msanii wa muziki,Ommy Dimpoz amesaini kufanya kazi na label kubwa ya muziki, RockStar4000 inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment
Muimbaji huyo kwa sasa ataungana na Alikiba ambaye alijiunga na label hiyo miaka 6 iliyopita, ambapo wiki iliyopita alitangazwa kuwa mmoja kati ya wamiliki wa label hiyo.
“Tanzanian Superstar singer-songwriter Ommy Dimpoz signed global exclusive management deal with #ROCKSTAR4000 & content deal #RockstarTV at the Rockstar Pan Africa Group HQ in South Africa,” ilisema taarifa hiyo ya RockStar4000.
Baada ya taarifa hiyo, Bongo5 ilimtafuta muimbaji huyo na kuamua kuzungumza naye mawili matatu kuhusu deal hiyo.
“Ni kweli nimesaini RockStar4000 kama ulivyosikia, kwahiyo kwa sasa nitakuwa nafanya kazi au kwa kifupi kazi zangu kuanzia sasa zitakuwa chini ya RockStar4000,” alisema Ommy Dimpoz.
“Nilikaa nao chini tukazunguma nikaona hili ni jambo zuri kwangu kwa sababu RockStar4000 ni kampuni kubwa duniani ambayo inafanya kazi za wasanii wengi sana. Kwahiyo PKP ikaona bora tufanye nao kazi ili kuupeleka muziki wa Ommy Dimpoz mbali zaidi. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili ya Ommy mwingine ambaye atakuwa na sura nyingine kabisa,” aliongeza Ommy Dimpoz.
Pia label hiyo nchini Tanzania inafanya kazi na muimbaji Lady Jay Dee pamoja na Baraka The Prince.
t.

No comments

Powered by Blogger.