HATIMAYE AJIBU ATAMBULISHWA RASMI KUWA MCHEZAJI WA YANGA, APEWA JEZI NO 10

Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imemtangaza rasmi Ibrahim Ajibu kuwa ni mmoja wa wachezaji wa timu hiyo watakaopambana kwenye kikosi chao kuanzia msimu ujao wa 2017/18.
Ibrahim Ajibu ambaye hucheza katika nafasi ya mshambuliaji anakuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na Yanga akitokea mikononi mwa watani wao, Simba kwa msimu huu wa 2017/18.  Ajibu ataitumikia Yanga kwa miaka miwili kama mkataba wake unavyosema.

Katika utambulisho huo, Ajibu amekabidhiwa jezi namba 10 mbele ya Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh na Husein Nyika ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga.

No comments

Powered by Blogger.