MANCHESTER UNITED YAKUBALI KUTOA PAUNDI MILIONI 75 KUMSAJILI LUKAKU

 Timu ya Manchester United imekubali kutoa dau la paundi milioni 75 kwa Everton ili kumnunua mshambuliaji Romelu Lukaku.
Lukaku, 24, ambaye ni mchezaji wa kimataifa raia wa Ubelgiji alifunga magoli 25 katika Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu uliopita.
United, ambayo ilikuwa ikimfukuzia Lukaku kwa majira yote ya kipindi cha uhamisho cha msimu wa joto, sasa haitamuhitaji tena Alvaro Morata kutoka Real Madrid.
Hatua ya kumnasa Lukaku haina uhusiano na mazungumzo yanayolenga Manchester United kumruhusu Wayne Rooney kwenda Everton.
Romelu Lukaku amekuwa akionekana akiwa mapumzikoni Marekani pamoja na Paul Pogba wa Manchester United

No comments

Powered by Blogger.