LEODEGAR TENGA ALA SHAVU CAF AUNGANISHWA NA KALUSHA BWALYA

Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Tenga, aliyewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF awali, atakuwa chini ya Rais Mzambia, Kalusha Bwalya kwenye Kamati hiyo.
Wote wawili, Rais na Makamu wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya CAF ni wachezaji na Manahodha wa zamani wa nchi zao, Tenga akicheza kama sentahafu na Bwalya ambaye pia ni Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Zambia (FAZ) alikuwa mshambuliaji.
Uteuzi huo umefanyika katika Mkutano Mkuu wa CAF Ijumaa mjini Rabat, Morocco.

No comments

Powered by Blogger.