Mganda Adakwa Dar na Paspoti 15 za Kusafiria!

          AishaTalib, raia wa Uganda akionyesha kwa wanahabari paspoti alizokamatwa nazo.

AISHA Talib, raia wa Uganda anayekadiliwa kuwa na umri kati ya 40, amekamatwa jijini Dar es Salaam akiwa na paspoti za kusafiria 15 za mataifa mbalimbali.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam (RIO), John Msumule akionyesha pasipoti walizozikamata.
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam (RIO), John Msumule amesema kuwa, Aisha walimkamatwa katika Hoteli ya Lamada iliyopo IIala ambapo anakabiliwa na makosa ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kibali, kuhodhi jumla ya paspoti 15 za raia wa nje ambapo 12 zimeonesha ni za raia wa Burundi na tatu za raia wa Madagascar ikisadikika kuwa wenye paspoti hizo wako Kenya huku wakitaka wapatiwe Visa za kwenda nchini Saudi Arabia.

                                   (RIO), John Msumule akionyesha pasipoti walizozikamata.
 Msumule aliongeza kuwa, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kesho na watuhumiwa wengine waliokamatwa na jeshi la uhamiaji, wakiendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani.
Alisema katika oparesheni waliyoifanya wamewakamata pia watuhumiwa wengine wakiwa wanaishi nchini bila vibali, wamiliki wa makampuni ya ulinzi yaliyoajiri watu wasiokuwa na sifa za kuishi nchini.
 Pia Kikosi cha uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza na kumchukulia hatua Mwenyekiti wa klabu ya Yanga na mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Group, Yusufu Manji kwa kosa la kuajiri wafanyakazi toka nje ya nchi wasiokuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria.

No comments

Powered by Blogger.