Manji Atakiwa Kujisalimisha Uhamiaji kwa Kesi Nyingine

DAR ES SALAAM: Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imemtaka mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa Quality Plaza, Yusufu Manji kuripoti uhamiaji mara baada ya kutoka hospitali alikolazwa.
Ofisa uhamiaji wa mkoa huo, John Msumule ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema Manji anatakiwa kufanya hivyo kwa kudaiwa kuwa ameajiri watu wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume cha sheria.
“Siku ya Ijumaa tulifanya upekuzi kwenye Jengo la Quality Plaza (linalomilikiwa na Yusuf Manji, lililopo Barabara ya Airport), tukakamata paspoti  126 ambapo paspoti 25 ndizo zina makosa, wamiliki wake hawana vibali  na wanafanya kazi kinyume na utaratibu, watapelekwa mahakamani pamoja na mwajiri wao, Yusuf Manji ili akajibu mashtaka hayo.
“Ilikuwa tumkamate jana lakini tukasikia kwamba amelazwa hospitali… hivyo akitoka hospitalini awasili haraka ofisi hii ili tumuunganishe kwenye kesi ya kuwaajiri watu wasio na vuibali….” Alisema Msumule.

No comments

Powered by Blogger.