MANCHESTER CITY YAKWEA HADI NAFASI YA PILI LIGI KUU UINGEREZA

Timu ya Manchester City imepanda hadi katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupambana na kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Bournemouth katika dimba la Vitality.

Akiwa ameanzia benchi mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero, aliingia katika dakika ya 14, kufuatia kuumia kwa mshambuliaji anayemyima namba kwa hivi sasa Mbrazili Gabriel Jesus.

Lakini alikuwa Raheem aliyeipatia Manchester City goli la kwanza, baada ya kipa Artur Boruc kuokoa mara mbili magoli, Tyrone Mings alijikuta akijifunga goli la pili kufuatia shinikizo la lililochangiwa na Aguero.
 Raheem Sterling akifunga goli baada ya kupokea pasi kutoka kwa David Silva
Mshambuliaji Gabriel Jesus akitolewa nje baada ya kuumia dakika ya 14 ya mchezo

No comments

Powered by Blogger.