MWANAMKE MWEUSI ATEULIWA KUWA MWANASHERIA MKUU NCHINI MAREKANI
Loretta Lynch ateuliwa kuwa mwanasheria mkuu nchini Marekani. |
Ikiwa uteuzi wake utaidhinishwa na bunge la seneti Loretta Lynch atakuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya afrika kuwa mkuu wa sheria nchini marekani .Uteuzi huo unafanyika wiki sita baada ya kujiuzulu kwa Eric Holder ambaye ndiye M'marekani wa kwanza mweusi kuteuliwa kuwa mkuu wa sheria nchini humo.
(Chanzo: BBC)
Post a Comment