Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) aliyechukua nafasi yake pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.
Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
Mrembo huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya
umri wake, jambo ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata)
kutokana na agizo la wizara husika kufuatilia ukweli wake. “Baada ya
kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali
dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema
wakati siyo,” amesema kwenye barua hiyo.
“Shutuma hizo
zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya
kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa
hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu
na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania
2014,” ameongeza.
“Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa
wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika
ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote
tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za
dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa
Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru
pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari,
Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”
“Leo
nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi
Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo
niliochukua.” (iliandikwa sehemu ya barua hiyo) Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamanzima.
| | | | | | | |
Post a Comment