RC Makonda atembelea Uwanja wa Fisi wanapofanya biashara ya ngono....Aahidi Kupavunja na Kujenga Viwanda Vidogovidogo

Jumapili Novemba 27 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam akiwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Akiwa katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa alipita katika viunga vya Kata ya Manzese na kutokea sehemu ambapo kula kilabu kinachouza pombe za kienyeji huku watu waliokuwa eneo hilo wakionekana kuwa wamelewa kiasi cha kutotambuana.

“Hii achana nayo kabisa ni moto wa kuotea mbali. Hebu niikate kidogo uone,” Mzee aliyefahamika kwa jina la Mandela alisikika akimtambia Paul Makonda huku akipiga funda la pombe hiyo ya kienyeji hali inayoonyesha kuwa hakuwa akifahamu kuwa anayezungumza naye ni Mkuu wa Mkoa.
Baadaye alienda eneo lenye vibanda vya chumba kimoja kimoja, amabavyo inaelezwa kuwa ni madanguro ambayo hutumika kufanyika biashara ya ukahaba hadi kwa wasichana wenye umri mdogo. Hata hivyo kila mlango aliojaribu kugonga ulikuwa umefungwa na hakuna aliyeitika na kufungua mlango.

“Hawa wakijua watu wa serikali wanakuja hapa basi hufunga biashara zote, sasa na hapa wamefunga, si rahisi kumpata mtu,” alisikika kijana mmoja mwenyeji wa eneo hilo akisema.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Tandale, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alisema serikali inafanya mipango ya kupata wawekezaji ili kununua eneo hilo la Uwanja wa Fisi na kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo ili vibanda vyote vivunjwe na kujengwa vitegauchumi badala ya kuliacha eneo hilo liharibu maisha ya vijana.

No comments

Powered by Blogger.