Rais Magufuli Atoboa Siri ya Kuivunjwa Bodi ya TRA
Rais John Magufuli
KUIDHINISHWA kwa Bodi ya Mamlaka ya
Mapato (TRA) kuweka mabilioni ya fedha katika benki binafsi ndiyo
sababu iliyomfanya Rais John Magufuli kuivunja bodi hiyo.
Rais Magufuli aliyasema hayo leo katika sherehe za mahafali ya Chuo
Kikuu Huria huko Kibaha Mkoa wa Pwani aliposisitiza kwamba TRA
walichukua mabilioni ya fedha na kuyaweka kwenye akaunti za muda maalum
(fixed accounts) katika benki nane ambapo bodi ikaidhinisha.Wiki iliyopita Rais Magufuli alivunja bodi hiyo na kutengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu bila kueleza sababu zozote.
Post a Comment