MFALME MOHAMED WA VI WA MOROCCO ATUA NCHINI KWA ZIARA RASMI YA SIKU TATU, APOKELEWA KWA SHANGWE NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI NA MAMIA YA WANANCHI

 Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI ( wa mbele) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
                   Mfalme wa Morocco Mohammed VI akipokea shada la maua
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Mfalme wa Morocco Mohammed VI wakisimama kwa nyimbo za Taifa.
 Mfalme wa Morocco Mohammed VI akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan kwa Mfalme wa Morocco Mohammed VI.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri Mkuu,Mh. Kassim Majaliwa  kwa Mfalme wa Morocco Mohammed .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika maongezi na mgeni wake Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI.
 Wafanyabiashara walioongozana na Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI

                                                                       PICHA NA IKULU

No comments

Powered by Blogger.