BONDIA FLOYD MAYWEATHER AJIRUSHA KATIKA PATI YA MARIAH CAREY

Bondia mstaafu Floyd Mayweather, ameonekana akijirusha na diva wa muziki wa Pop Mariah Carey katika sherehe mwanamuziki huyo ya mwaka ya Halloween.



Mayweather ambaye alijiuzulu akiacha rekodi ya kutopigwa, alionekana akipozi kupiga picha akiwa na Mariah, ambaye alikuwa amevalia nguo nyekundu ya shetani yenye kubana.



Akiwa ni mwenyeji wa sherehe hiyo Mariah Carey alionekana kuwa kivutio kwa wageni aliowaalika huku akijimwaya na gauni lake hilo la shetani mwekundu.
                        Mariah Carey akiwa amepozi na bondia Floyd Mayweather.

No comments

Powered by Blogger.