Polisi akikamata haulizi itikadi ya mtu - Mwigulu
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema Jeshi la Polisi
nchini linafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu na linapomkamata
mtu halimuulizi itikadi ya chama chake.
Waziri
Mwigulu ameyasema hayo leo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) kutoka Mwanza Susan Masele aliyetaka
kupata kauli ya serikali juu ya askari polisi ambao wanawabambikizia
kesi wafuasi wa UKAWA kwa kuwapa kesi za uchochezi.
“Jeshi
la polisi linapowakamata watu, haliwaulizi itikadi zao, na
linapowafikisha mahakamani haliwaulizi kadi za vyama vyao bali huangalia
kosa ambalo limefanyika” Amesema Waziri Mwigulu.
Aidha
waziri amesema kuwa wananchi wanaweza kupeleka malalamiko yao kuhusu
Jeshi la Polisi katika vyombo vinavyoshughulikia sheria au katika makao
makuu ya jeshi kwa kuwa kuna kitengo kinachoshuhulikia malalamiko ya
wananchi.
Sambamba
na hayo Waziri Mwigulu ameweka bayana kwamba askari ambao hukutwa na
mashtaka ya kuwabambikizia wananchi kesi au mambo mengine na yakibainika
kuwa ni ya kweli huadhibiwa na kulingana na sheria.
Post a Comment