LIONEL MESSI KUUKOSA MCHEZO WA ARGENTINA DHIDI YA VENEZUELA
Mchezaji
Lionel Messi atakosa mchezo wa kuwania kufuzu kutinga fainali za
kombe la dunia baina ya Argentina na Venezuela, baada ya kuumia
katika mchezo wa Alhamisi dhidi ya Uruguay.
Mshambuliaji
huyo wa timu ya Barcelona, aliumia nyonga katika mchezo huo aliofunga
goli moja lililoipa ushindi Argentina, baada ya kuamua kubadili
uamuzi wake wa kustaafu kuichezea timu ya taifa.
Post a Comment