KOCHA ARSENAL ARSENE WENGER KUTOSOMA KITABU CHA HASIMU WAKE JOSE MOURINHO
Kocha Arsenal, Arsene Wenger,
amesema hatosoma kitabu cha kocha mwenzake wa Manchester United, Jose
Mourinho, ambacho amenukuliwa akisema atauvunja uso wa kocha huyo
Mfaransa.
Jose Mourinho amekuwa mara kwa mara
akigombana na Wenger wakati alipokuwa na Chelsea, na aliwahi
kumueleza Wenger kuwa atakuja kuwa mtu spesho wa baadaye.
Alipoulizwa iwapo atasoma kitabu
hicho Wenger amesema hayupo katika muda wa kuharibu, kwani kwa sasa
anatilia mkazo kujiimarisha na mchezo wao wa jumamosi dhidi ya Chelsea.
Mourinho, 53, aliwahi pia kumuelezea
Wenger sawa na mla chabo (kozi), mwaka 2005 baada ya Mfaransa huyo
kuhoji sera za uhamisho wa Chelsea.
Post a Comment