Mtoto Aishi Porini Siku Tatu
mtoto baada ya kuokolewa.
Mtoto huyo akiwa na mama yake.
RUSSIA: Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu, Tserin Dopchut ameishi pekee yake kwa muda wa siku tatu mfulululizo ndani ya misitu minene ya Siberi yenye baridi kali sambamba na wanyama wakali jamii ya Dubu na Mbwamwitu.
Mtoto huyo alipatikana akiwa salama bila kupatwa na madhara yoyote kutoka kwa wanyama hao.
Akiwa porini mtoto huyo alikuwa akishindia biskuti aina ya chocolate ambazo aliondoka nazo nyumbani kwao siku alipotoweka.
Baada ya kupatikana mtoto huyo cha kwanza aliuliza ulipo mdoli wake wenye muundo wa gari.
Ayas Saryglar, Mkuu wa kikosi cha uokoaji kwenye misitu hiyo minene ameliambia jarida la Siberian Times:
“Kuna Mbwamwitu na Dubu. Kipindi hiki wanyama wote wanajificha kutokana na baridi kali, wanaweza kudhuru kiumbe chochote kinachokatiza mbele zao. Kifupi hali ya mtoto ilikuwa hatarini.” Alisisitiza.
Na Leonard Msigwa/GPL/MTANDAO.

Post a Comment