Basi la New Force Lapata Ajali na Kuua Watu 12
Watu
12 wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi
la kampuni ya New Force kupinduka katika eneo la Ilongwe kata ya
Kifanya, Mkoani Njombe na kupelekea vifo hivyo pamoja na majeruhi.
Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mkoa wa Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kumakia leo wakati likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe.
Katika
tukio lingine la ajali iliyotokea mkoani Kilimanjaro katika msafara wa
ziara ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki imesababisha
majeruhi wawili akiwemo afisa wa polisi pamoja na mwandishi wa habari wa
shirika la habari la taifa ambao wote wamelazwa kwa ajili ya matibabu.
Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mkoa wa Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kumakia leo wakati likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe.
Kwa
mujibu wa habari iliyotolewa na shirika la habari la taifa kutoka
mkoani Njombe zinasema kati ya watu hao 12 wanawake ni nane akiwemo
mtoto mmoja wa kike pamoja na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa
kiume.
Mmoja
wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo
kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari
basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka
kabisa.
Post a Comment