ZARI ADAIWA KUTISHIA KUTOA MIMBA!

                                                              Zarinah Hassan ‘Zari 
Stori:  Musa Mateja, Ijumaa

DAR ES SALAAM Hakuna ubishi kuwa mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ni mjamzito lakini habari ambayo hujaisikia ni kwamba hivi karibuni mwanamama huyo alidaiwa kutaka kuichoropoa mimba hiyo kisa lynn.

                                                                     Irene Hilary ’Lynn
Chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu wa Diamond kilitumwagia ubuyu kuwa, baada ya yale madai kuwa Diamond anatoka na yule Video Queen wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Irene Hilary ’Lynn’, Zari alimaindi kinoma na kufikia hatua ya kutaka kuitoa mimba ili kumkomoa Diamond.

Inadaiwa kuwa, kilichomkasirisha zaidi Zari ni kitendo cha mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuonesha kufurahia kitendo cha mwanaye kumsaliti.
                                                                    Diamond na Zari
“Ninyi hamjui tu jinsi ile skendo ya Diamond kutoka na Lynn ilivyotaka kuleta balaa, unaambiwa Zari alitishia kutoa mimba, mbaya zaidi ni pale zilipoibuka tena taarifa kuwa, Lynn ana mimba, mbona ulikuwa mtiti?” kilidai chanzo hicho.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa, kutokana na hali hiyo, Diamond alitumia nguvu kubwa kumsihi mzazi mwenzake huyo kutosikiliza maneno ya watu na badala yake aitunze mimba hiyo ili amzalie mtoto wa pili baada ya Tiffah ambaye sasa ana umri wa mwaka mmoja.
Madai hayo yalimfanya paparazi wetu amtafute Diamond ‘Baba Tiffah’ kwa njia ya simu kuyazungumzia ambapo alipopatikana alisema: “Unajua uhusiano una changamoto nyingi sana lakini ninachoweza kushukuru ni kwamba leo hii mimba ya baby wangu ina zaidi ya miezi minne na Mungu akijaalia mwezi Desemba nitapata mtoto mwingine wa kiume, hayo mengine tuyaache.”

Akaongeza: “Unajua watu wanaongea sana hasa kwenye mitandao ya kijamii lakini sisi ni waelewa na hatuwezi kuwapa watu nafasi watuharibie.”

Diamond na Zari wamekuwa kwenye uhusiano wenye figisu nyingi huku wengine wakidai hawawezi kudumu kutokana na msanii huyo kudaiwa mara kadhaa kusaliti ambapo skendo mbichi inayomtafuna ni ya kuwapachika mimba Lynn na modo Hamisa Mobeto.

No comments

Powered by Blogger.