MAHABUSI WALIOJARIBU KUTOROKA WATIWA MBARONI
Mahabusi
wawili kati ya saba waliotoroka chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la
Polisi katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro,
wametiwa mbaroni na kuhukumiwa kutumikia vifungo jela.
Kutoroka kwa mahabusi hao kulisababisha askari 10 mkoani Kilimanjaro waliokuwa wakiwalinda kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Mahabusi
hao ni Lucas Akaro (26) ambaye alijisalimisha kwa uongozi wa Gereza la
Karanga na Charles Malenge (24), aliyekamatwa na Polisi akiwa amejificha
nyumbani kwake.
Wakati
wakitoroka, Akaro alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji ya mwanafunzi
wa mwaka wa tatu chuo cha udaktari KCMC, Baneti Materu (22) na Malenge
ya unyang’anyi.
Mahabusi
hao walifikishwa kortini jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Joachim
Tiganga na kukiri shtaka moja kati ya mawili yaliyokuwa yakiwakabili.
Post a Comment