DK. KIGWANGALA ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMKAMATA NA KUMFIKISHA MAHAKAMANI JUMA MWAKA WA FOREPLAN (T) LIMITED KWA KUKIUKA SHERIA ZA NCHI
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akiwa nje ya Jengo la Kituo cha
Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED mara baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza kufuatia mmiliki wa kituo hicho Tabibu Juma
Mwaka kuendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa kwa siri pia kujitangaza
kwenye vyombo vya habari licha ya agizo la Serikali la Julai 11, 2016 la
kumtaka asitishe kutoa huduma zake kutokana na kukosa vigezo vya
kisheria vya kumruhusu kutoa tiba nchini.
Baadhi
ya Wagonjwa waliokutwa wakisubiri Tiba katika kituo cha Tiba Asili na
Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopigwa marufuku na Serikali
kutoa huduma zake nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akizungumzwa na baadhi ya
wafanyakazi wa kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T)
LIMITED waliokuwa wakitoa huduma licha ya kituo hicho kupigwa marufuku
na Serikali kutoa huduma zake nchini.Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri
Dkt. Hamis Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata ndani ya saa
24 na kumfikisha Mahakamani Mmiliki wa Kituo hicho tabibu Juma Mwaka
kwa kukiuka agizo la Serikali na kutoa huduma kinyume cha Sheria.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia), Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M
.Swebe (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala
Dk. Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) kwa pamoja wakipitia kwa makini
baadhi ya nyaraka zilizokutwa ndani ya kituo cha Tiba Asili na Tiba
Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia
upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam
kwa lengo la kuchukua vielelezo kama ushahidi wa Tabibu Mwaka
kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria.
Post a Comment