Godbless Lema Agoma Kula Kwa Saa 48
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema ( Chadema) anayeshikiliwa katika
mahabusu ya kituo kikuu cha Arusha Mjini amegoma kula kwa zaidi ya saa
48 sasa tangu alipokamatwa
Lema
alikamatwa juzi alfajiri akiwa nyumbani kwake Njiro Arusha kwa tuhuma
za kutoa maneno ya uchochezi na kushawishi watu kwa njia ya mtandao
waandamane Septemba mosi.
Jana Meya wa Arusha, Calist Bukhay alisema Lema amegoma kula
Alisema
Lema aligoma kula akidai kuwa alifanyiwa udhalilishaji mbele ya watoto
wake wakati polisi walipokuwa wakitekeleza agizo la kumkamata.
"Ni
kweli amegoma kula tangu jana (juzi) alipokamatwa.Alisema askari polisi
walipkwenda kumkamata walimfanyia vitendo vya udhalilishaji mbele ya
watoto wake na kumnyanyasa bila kujali yeye ni kiongozi wa wananchi.
"Sasa
yeye ameshikilia msimamo wake kuwa kwa kuwa polisi walikuwa wamepanga
kumuua wakati wa kumkamata, basi ni bora akafa kwa njaa.
"Chakula
kimekuwa kikipikwa na kupelekwa na mkewe ,lakini bado amegoma
kukila.Baada ya tukio hilo, polisi walituita ili kujaribu kumshawishi
ale mchana, akagoma" Alisema Meya Calist.
Post a Comment