WAZIRI NCHEMBA AMTEMBELEA GEREZANI KIJANA ALIYEDAIWA KUTESWA NA WACHINA HUKO GEITA, AAMURU WAHUSIKA KUTIWA MBARONI.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi huku kubwa likiwa ni kufuatilia kuenea kwa taarifa na picha za mateso kijana wa Kitanzania yanayodaiwa kufanywa na raia wa Kichina wanaomiliki sehemu ya Mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro - Geita, ambaye alikuwa ni mfanyakazi katika Mgodi huo.

Waziri Mwigulu alilazimika kufanya ziara hiyo ambapo alikwenda moja kwa moja Gereza la Geita ili kukutana na kijana huyo ambae yupo hai tofauti na taarifa za awali kuwa alifariki, na baada ya kujiridhisha kuanzia mavazi, majeraha, picha, sura na umbo lake kuwa ndiye kijana aliyeteswa vibaya na picha zake kusambaa mitandaoni na vyombo mbalimbali vya habari, aliamua kumchukua kijana huyo na kuongozana nae kwenda hadi mahala ulipo mgodi huo lilipofanyika tukio hilo la kinyama, ambapo kijana huyo alitakiwa kuwatambua wahusika ambao nao inadai ni kweli walihusika kufanya tendo hilo la kinyama kwa kijana huyo.

Kufuatia utambuzi huo na maelezo ya wahusika, Waziri Nchemba aliagiza wahusika wakamatwe mara moja ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kwa wahusika hao.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akiwa nje ya Gereza la Wilaya ya Geita, alikowekwa ndani kijana huyo baada ya kufanyiwa tukio hilo la kunyanyaswa na Mabosi wake hao ambao walimshtaki kuwa ni mwizi.
     
     Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimuangalia kijana huyo na                            kujiridhisha kuwa ni yeye aliepatwa na Mkasa huo.


                           Baadhi ya Wachina wanaofanya kazi katika Mgodi huo wakiwa nje.
                            Sehemu ya Watuhumiwa wa tukio hilo wakiwa chini ya Ulinzi.

No comments

Powered by Blogger.