TUNDA AFUNGUKA KUMWAGANA NA YOUNG D
MAYASA MARIWATA
MUUZA nyago macha-chari Bongo, Tunda Sebastian amefunguka
kumwagana na mwandani wake wa muda mrefu, ambaye ni staa wa Bongo Fleva, David
Genzi ‘Young D’ na kusema ameamua kujiweka kando kwenye maswala ya mapenzi.
Akipiga stori na Showbiz Xtra baada ya kumbananisha
kuhusiana na tetesi za uhusiano wake kuvunjika kutokana Young D kubaini anatoka
na mwanamuziki mwenzie (jina kapuni) ndipo akaeleza kuwa, ishu hiyo haina
ukweli ila ameachana na mwandani wake huyo kwa sababu ambazo hawezi kuzianika
kwa sasa.
“Hayo ya kutoka na huyo msanii si kweli na kuhusu Young D
nimeshaachana, sifikirii kuwa na msanii yeyote na sihitaji mpenzi kwa sasa,”
alisema.
Post a Comment